Hivi karibu msanii Mbosso Khan ameviteka vichwa vya habari kwa burudani yake ndani ya Simba Day pamoja na maandalizi yake baada ya kuutumia ubunifu wa movie pendwa “Mad Max; fury Road”
Movie ambayo imebeba ubunifu wa aina yake ambao msanii huyo aliamua kuutumia, Director wa video hiyo maarufu Fole X kwenye mahojiano na kipindi cha The Switch ya Wasafi Fm amefunguka gharama zilizotumika kutengeneza video ile ambayo ilizua taharuki baada ya Mbosso, kuonekana ameteleza na kuangukia baharini.
Director licha ya kutoweka wazi kiasi kilichotumika ameweka wazi kuwa kama Mbosso angeamua kutengeneza video basi angetengeneza video sita za nyimbo. Zaidi, kasema Mbosso katumia watu zaidi ya 300, kufanikisha ubunifu ule.
Ifahamike, Mad Max Fury Road ni moja kati ya movie zenye bunifu nyingi za aina yake ndani mbali na zile za kitaalamu lakini magari ya ajabu pamoja na mionekano ya watu ndio kitu kina kosha watu wengi na vitu hivyo ndio msanii Mbosso aliamua kuvitumia kuipamba Simba Day ya 2025/26.
Chanzo; Tanzania Journal