Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Godmother wa Rapa 2pac Afariki Dunia, Mtu wa Harakati

Assata Shakur, mwanachama mashuhuri wa Jeshi la Ukombozi Weusi (Black Liberation Army), na “godmother” wa rapa 2pac Shakur, afariki ambapo aliaga dunia Septemba 25, 2025 huko Havana, Cuba, akiwa na umri wa miaka 78 ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba imetangaza kifo chake Septemba 26,2025, taarifa ikisema kifo chake kimetokana na magonjwa ya kiafya pamoja na uzee, kifo chake kimethibitishwa na mwanae Kakuya Shakur, kupitia mitandao ya kijamii.

Assata, Alizaliwa kama JoAnne Deborah Byron Julai 16, 1947, alijulikana pia kama Joanne Chesimard. Alikuwa mtetezi wa mapinduzi ya silaha dhidi ya ubaguzi nchini Marekani, na alihusishwa na Chama cha Black Panther. Mnamo 1973, alihusika katika tukio la risasi kwenye Turnpike ya New Jersey, ambapo askari wa serikali Werner Foerster aliuawa, na yeye kujeruhiwa. Alidai kuwa FBI walikuwa wamemlenga kama sehemu ya kampeni dhidi ya viongozi wa kupambana na ubaguzi wa rangi katika miaka ya 1960 na 1970.

Ilipofika mwaka 1977, alipatikana na hatia ya mauaji ya Foerster na akahukumiwa kifungo cha maisha jela. Alitoroka jela huko New Jersey mnamo 1979, akisaidiwa na wenzake wa BLA na May 19th Communist Organization na 1984, alipata hifadhi ya kisiasa kutoka kwa Fidel Castro nchini Cuba, ambapo aliishi hadi umati wake ulipomkuta.

 Zaidi, Anafahamika kama “godmother” yani mungu mama wa rapa Tupac Shakur, ambaye aliuawa mnamo 1996, pia  shangazi yake wa kambo. Mama yake, Afeni Shakur, alikuwa rafiki wa karibu na Assata katika harakati za Black Panther.

Na 2013, FBI ilimweka kwenye orodha yake ya magaidi wanaotafutwa zaidi, akiwa mwanamke wa kwanza hapo. Pamoja na Wakili wa Jimbo la New Jersey, waliongeza zawadi ya kukamatwa kwake hadi dola milioni 2. Hifadhi yake nchini Cuba ilizua migogoro, na wengine wakidai kuwa Cuba inapaswa kubaki kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: