Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Vitu Dunia Inaongea Kuhusu 2pac

Dunia imeshuhudia watu maarufu wengi ambao waliitikisa kwa umaarufu hata kabla ya kuondoka ulimwengu, Tupac Shakur, 2Pac , ambaye ni moja ya nyota kubwa kuwahi kung’aa kwenye historia ya muziki wa hip hop duniani huwezi acha kuliweka jina lake kwenye kapu hilo na kila ifikapo Septamba 13 ya kila mwaka dunia na wanahiphop ni kumbukizi ya kifo chake. Alizaliwa Juni 16, 1971 na kuaga dunia Septemba 13, 1996, baada ya kupigwa risasi huko Las Vegas.

 Na kila ifikapo kumbukizi ya kifo cha rapa huyo makini kuwahi tokea mjidala na mazungumzo mbalimbali mapya na ya zamani uibuka dhidi ya rapa huyo, pita kidogo kwenye dodoso chache ambazo dunia inazungumza kuhusu 2pac

Alizaliwa East Coast yani New York lakini mwenye mapenzi ya damu na West Coast, Zaidi, inafahamika kuwa 2pac alikulia kwenye familia yenye migogoro.

 Alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Madonna, lakini ulivunjika kwa sababu

za kirangi yani ubaguzi warangi kati ya wazungu na mablack amerika ulisambalatisha mahusiano yao.

Pia inadiwa kuwa  Baada ya kifo, mwili wake ulichomwa moto, na wafuasi wake wa kundi la Outlawz walichukua majivu yake, wakayachanganya na bangi na kuvuta

Unaambiwa 2pac sio rapa tu. Nyimbo zake kama Changes, Dear Mama, na California Love, zina maana kubwa kijamii kwani amegusa sana maisha ya umaskini, ubaguzi wa rangi, na maisha ya uhuni “Genge” kupitia uwandishi wake. Kwenye moja mahojiano 50 Cent aliwahi sema "2Pac alikuwa kama kamera kila line ilikuwa hatari”

Kifo chake na cha Notorious B.I.G. kimeongeza hadhi yao kama malegends huku umma ukisema vifo vya wawili hao m vinewaongezea umaarufu zaidi kuliko enzi za uhai wao.

 Snoop Dogg, kwa sasa ndiye anayetajwa kama rafiki mkubwa wa 2pac katika kizazi hiki kuliko yeyote.

Ni miaka 29 tangu kifo chake Septemba 13, 1996, Kuna nadharia zemeibuliwa zinazodai kuwa alihifadhiwa mahali pa siri na wengi bado wanaamini 2Pac yuko hai na atarejea 2030.

Kwa ufupi, Dunia inamkumbuka 2Pac kama nguri au gwiji wa hip-hop, mshairi aliyezungumzia changamoto za jamii, ambaye kifo chake kimeongeza hadhi ya ulegend wake kwa yale aliyoyafanya kwenye ulimwenguni yani kijana aliyeondoka duniani mapema aliyeacha kafanya makubwa hasa kupitia nyimbo zake na maisha yake kwa ujumla.

 

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: