Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwigizaji Eric Dane Afariki Dunia Akiwa Amezungukwa na Wependwa

Mwigizaji maarufu wa Marekani, Eric Dane amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kupambana na ugonjwa wa ALS (Amyotrophic Lateral Sclerosis) ambapo taarifa kutoka kwenye familia yake zimeeleza kuwa Eric alifariki akiwa nyumbani na akiwa amezungukwa na Wapendwa wake ikiwa ni mwaka mmoja tangu atangaze hadharani kuwa anasumbuliwa na ugonjwa huo wa neva unaoathiri misuli na uwezo wa mwili kufanya kazi kawaida.

Eric Dane alijipatia umaarufu mkubwa duniani kupitia nafasi yake ya Dk. Mark Sloan maarufu kama “McSteamy” katika tamthilia ya hospitali ya Grey’s Anatomy, uigizaji ambao uliifanya nafasi hiyo kuwa miongoni mwa Wahusika waliopendwa zaidi katika historia ya tamthilia hiyo na kisha baadae alionekana pia katika tamthilia ya kijeshi ya The Last Ship, ambapo aliigiza kama Kamanda Tom Chandler.

Katika miaka ya karibuni, alirejea kwenye uigizaji kwa mafanikio makubwa kupitia tamthilia ya HBO Euphoria akiigiza kama Cal Jacobs nafasi ambayo ilimletea sifa mpya na kumtambulisha kwa kizazi kipya cha Watazamaji ambapo mbali na televisheni, Dane alishiriki pia katika filamu kadhaa za Hollywood zikiwemo X-Men: The Last Stand ambako aliigiza kama Multiple Man, pamoja na Valentine’s Day.

Pumzika kwa amani Bingwa 🙏🏿 nilikukubali sana kwenye THE LAST SHIP.

 

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: