Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kazi za Michael Jackson Zaendelea Kuingiza Mabilioni

Ni miaka 16 sasa tangu kutokea kifo cha Mfalme wa Pop, Michael Jackson ‘MJ’ aliyefariki dunia Juni 25, 2009 jijini Los Angeles, Marekani. Lakini licha ya kifo chake bado matunda ya kazi zake yanaonekana.

Kwa kujibu wa taarifa iliyotolewa na jarida la Forbes, inaelezwa kuwa kazi zake zote za sanaa zimeingiza zaidi ya dola 3.5 bilioni tangu alipoaga dunia. Ambapo hatua hiyo imemfanya kuweka rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na msanii yeyote aliyefariki.

Inaelezwa mara tu baada ya taarifa ya kifo chake, albamu zake kama Thriller, Bad na Dangerous zilirudi tena mjini na kupata mauzo zaidi ya yale ya mwanzo. Huku filamu yake ya 'This Is It', ikivuna zaidi ya dola milioni 260 katika kumbi za sinema.

Aidha baada ya mauzo hayo kuongezeka kwa kasi. Zaidi ya wasimamizi wa mali za Michael Jackson Estate waliamua kujipanga katika kutangaza kazi hizo katika sinema, mitandao ya kijamii pamoja na redioni kuhakikisha jina lake linaendelea kufanya vizuri kibiashara bila kupoteza heshima yake.

Hata hivyo mwaka 2016 ulitajwa kuwa mwaka wa kihistoria MJ Estate baada ya kuuza hisa zake kwenye kampuni ya Sony/ATV kwa dola milioni 750, pamoja na kununua haki miliki za muziki wa MJ kwa takribani dola milioni 600-800.

Kutokana na hayo MJ amekuwa akiingiza dola milioni 100 hadi 400 kila mwaka baada ya kufariki kiasi kinachoendelea kumuweka katika nafasi nzuri huku akishika namba moja Forbes ya watu waliofariki lakini wanaingiza fedha nyingi zaidi.

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: