Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Sababu za Taylor Swift Kutotinga Grammy 2026

Mkali wa muziki wa Pop, Taylor hajaorodheshwa kwenye Tuzo za Grammy 2026 jambo lililowashangaza baadhi ya mashabiki wa muziki wake.

Hata hivyo, inaelezwa chanzo cha kutokuwepo kwenye kinyang’anyiro chochote licha ya kufanya vizuri mwaka huu si kwa sababu amepuuzwa na kamati ya Grammys bali hakustahili kushiriki katika mchujo wa mwaka huu.

Iko hivi; baada ya tangazo rasmi la majina ya waliochaguliwa kutolewa Novemba 7, 2025, mashabiki wengi walihoji ni kwa nini albamu yake mpya The Life of a Showgirl, iliyotoka Oktoba 3, 2025 haikuonekana kwenye orodha ya wagombea. Ukweli ni kwamba, Taylor alitoa albamu hiyo nje ya dirisha la kusajili kazi lililowekwa na Recording Academy.

Kwa mujibu wa kanuni rasmi za Grammy, kazi za muziki zinazotaka kuwania tuzo lazima ziwe zimetolewa ndani ya kipindi cha kustahili cha mwaka husika.

Kwa mwaka huu, dirisha hilo lilianzia Agosti 31, 2024, na kuisha Agosti 30, 2025. Kwa kuwa albamu hiyo iliachiwa Oktoba 3, 2025 ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja baada ya muda huo, haikuruhusiwa kushiriki kwenye mchujo.

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: