Ushirika wa Emoji duniani umetoa list ya emoji 19 mpya ambazo zitatoka mwaka huu.
Baadhi ya emoji mpya ambazo zimetajwa ni:
◎ Uso wa kukunja macho (squinting face)
◎ Ishara ya kidole gumba kikielekea upande wa kushoto 👉 na kulia 👈
◎ Kipepeo aina ya monarch
◎ Tango lililochachushwa (pickle)
◎ Mnara wa taa za baharini (lighthouse)
◎ Kimondo (meteor)
◎ Kifutio cha penseli (eraser)
◎ Wavu wa kukamata wadudu (bug net)
Emoji hizi zitaanza kutoka mwezi wa tisa mwaka huu kwa watumiaji wa simu, kompyuta, internet na platform zote ambazo zinakubali mfumo wa emoji.
Chanzo; Clouds Media