Kristy Scott ni influencer maarufu wa mitandao ya kijamii hasa Tiktok wa nchini Marekani ambaye amewasilisha ombi rasmi la talaka kutoka kwa mumewe Desmond Scott katika Mahakama ya Harris County jijini Texas nchini humo.
Katika nyaraka za talaka, Kristy aliweka sababu ya talaka kuwa ni kutotendewa haki na kukosekana kwa uaminifu (alleged infidelity) akidai kuwa mumewe huyo hakuwa mwaminifu hivyo kusababisha uhusiano wao kuzama kiasi cha kukosa matumaini ya kuendelea kuwa pamoja.
Wawili hao walianza uhusiano walipokuwa vijana na kufunga ndoa mwaka 2014 baada ya miaka mingi ya kukutana na kuishi pamoja ambapo wamejaliwa watoto wawili, Vance na Westin.
Kufuatia sakata hilo, Desmond ameweka ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram akisema anasikitika juu ya jambo zima na kwamba alifanya “maamuzi ambayo hajivuni nayo” mwishoni mwa uhusiano wao, bila kueleza kwa kina.
Alisema pia ataendelea kuwa baba anayejali watoto wao na anaomba faragha na huruma wakati wanajipanga kufikia sura hiyo mpya ya maisha yao.
Wawili hao walijulikana sana kama wanandoa maarufu wa mitandao ya kijamii, wakipost maudhui ya maisha yao ya kila siku, vichekesho na maisha ya familia na walikuwa na wafuasi wengi, zaidi ya mamilioni TikTok, Instagram na YouTube.
Chanzo; Global Publishers