Veronica Mathias, Dada wa marehemu mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili, aliyefariki dunia Novemba 16, 2025 jijini Dodoma, amesema kuwa siku ya jana baada ya familia kupata taarifa za kifo chake walishindwa kufika hospitalini kutokana na kuwa na majukumu mengi. Hivyo, hawakupata nafasi ya kuuona mwili mara moja, lakini walioupata kuona awali walieleza kuwa mwili huo ulikuwa na alama zinazofanana na majeraha.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, 2025 nyumbani kwa marehemu eneo la Swaswa jijini Dodoma, ambako msiba unaendelea, dada huyo amesema kuwa walipofika hospitalini leo asubuhi wamejiridhisha kuwa mwili wa MC Pilipili ulikuwa na majeraha yanayoonekana.
Kufuatia sintofahamu hiyo, Tumempigia simu Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gallus Hyera kuhusu chanzo rasmi cha kifo chake ambapo amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi na watatoa taarifa rasmi.
Chanzo; Clouds Media