Msanii na mjasiriamali Zuwena Yusuphu Mohammed, Shilole, amepata ajali mbaya ya gari usiku wa kuamkia leo eneo la Malagarasi mkoani Kigoma alipokuwa safarini kutoka Kigoma kwenye mwaliko wa sherehe za mwaka mpya aliopewa na Mbunge wa Kigoma mjini.
Taarifa za ajali zimethibitishwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Cleyton Chipando, Baba Levo, ambaye ameandika "JANA USIKU DADA YANGU SHILOLE ALIPOKUWA ANATOKA KIGOMA KURUDI DODOMA ALIPATA AJALI YA GARI AINA YA ALPHAD BAADA YA KUGONGA NG'OMBE MAENEO YA MARAGALASI ..!! TUNAFATILIA AFYA YAKE KWA UKARIBU KWA SASA ANAENDELA KUPATA MATIBABU TABORA"
Chanzo; Clouds Media