Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ifunanya Afariki Baada ya Kuumwa na Nyoka

Msanii Ifunanya Nwangene aliyefahamika zaidi kupitia ushiriki wake katika Msimu wa 3 wa shindano la muziki la “The Voice Nigeria” ameripotiwa kufariki dunia baada ya kuumwa na nyoka.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya Nwangene kuumwa na nyoka hali iliyopelekea afya yake kuzorota kabla ya kufariki dunia.

Mpaka sasa maelezo zaidi kuhusu mazingira kamili ya tukio hilo bado hayajawekwa wazi.

Kifo chake kimeibua huzuni kubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki, wasanii wenzake na wadau wa burudani nchini Nigeria ambao wameendelea kutoa salamu za rambirambi na kumbukumbu za heshima kwa msanii huyo.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: