Rapa wa Marekani Fetty Wap amerejea nyumbani rasmi Januari 8,2026 baada ya kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka mitatu gerezani kati miaka 6. Fetty alitarajiwa kutoka gerezani Disemba 8, 2026, kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanywa Novemba 14, mwaka uliopita.
Fetty Wap alihukumiwa kifungo cha miaka 6 jela katika gereza la FCI Sandstone, Minnesota huko nchini Marekani Mei, 2023 baada ya kukiri kosa la kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya. Ripoti zinasema kuwa sasa amehamishwa hadi kwenye kifungo cha nyumbani huku akimaliza kifungo chake kilichosalia.
Fetty Wap ambaye jina lake kamili ni Willie Junior Maxwell II alizaliwa Juni 7,1991 Paterson, New Jersey nchini Marekani. Anafahamika kwa ngoma kama “Trap Queen,” iliyotoka mwaka 2015 na kufanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye chart kubwa za muziki Billboard Hot 100 sambamba na kuwateuliwa kuwania tuzo za Grammy mwaka 2016 kwenye vipengele viwili; Best Rap Song na Best Rap Performance.
Chanzo; Crown Media