Lamata Mwendamseke, anayejulikana pia kama 'Lamata Leah amezungumzia urafiki wake na mwigizaji Kajala nakusema kuwa walifahamiana kati ya mwaka 2013 na 2014 baada ya Kajala kutoka gerezani. Uhusiano wao ulikuwa kupitia kazi, huku mwigizaji Wolper akichangia kuwaunganisha.
Lakini pia Lamata amemsifia Kajala kwa usafi wake nakusema haoni mwanamke wa kumlinganisha nae.
"Kajala ni msafi kupita kiasi, sijawahi kukutana na mwanamke anayemzidi katika usafi. Mpaka sasa bado natafuta mtu anayefikia viwango vyake," amesema Lamata
Stori hii inapatikana kwenye ukurasa rasmi wa Mwananchi Scoop.