Kadri miaka inavyozidi kusonga vijana wa kisasa maarufu Gen Z, wamekuwa wakiibuka na namna mbalimbali za kuishi na namna ya kupambania ndoto na hatima ya maisha na ndoto zao, wapo wanaoshangazwa na namna wamechagua na wapo wanao ona sawa.
Lakini mwanamuziki wa kizazi kipya nchini, Salaman Ismail Hoza, Maarufu Kusah, ameshangazwa na hali ya vijana wa siku hizi huko kijijini kwao, Bumbuli, Lushoto, Tanga, kujikita zaidi kwenye ulevi dhidi ya kufanya maisha hasa wakishafikisha miaka 18.
Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maarufu cha radio Xxl ya Clouds Fm September 26,2025, amefunguka kwa hisia kuhusu vijana hao na lengo la yeye kwenda kuzindulia Ep yake inayofanya vizuri kwa sasa mtaani na hata kwenye majukwaa ya kidijitali “Bumbuli Boy.”
“Tulikuwa na semina tunaongea na vijana wadogo, ni sehemu wakati nipo vijana walikuwa wema lakini sasa hivi 70% ya vijana wanakunywa pombe ni walevi. Nafikiri hakuna watu wa kuelimisha kama kila kitu kinawezekana”
“Wengine wanaamini wakifikisha miaka 18 ni mtungi tu baada ya kujua miaka hiyo ikifika inabidi tutimize ndoto zetu, nimeapelekea hichi kitu waone vitu vinawezekana.” - Kusah
Zaidi, akaweka wazi juu ya muendelezo wake wakusaidi watu wenye mahitaji kama alivyoanza na Godfrey Mteule, kijana aliyemtoa kigoma na kufanikisha kufanya naye wimbo mmoja “Huyu Mungu” na baada ya hapo kuusimika utaratibu huo kama desturi nduguze Bumbuli.
Chanzo: Tanzania Journal