Licha kudumbukia kwenye dimbwi ambalo limemeza wengi walioweza kutoka na walioshindwa kutoka, Msanii Chid Benz akiwa anaelekea kutimiza miaka 40 akiri kutojutia aliyoyapitia angali bado yuko hai na uraiani.
Huku akitolea mfano majina makubwa yakiyotikisa kiwanda muziki Duniani na msoto wanaopitia kushinda hata yeye licha ya watu hao kua na pesa nyingi kumzidi.
“Hakuna kitu najuta mimi naishi maisha nagundua kuwa mimi sio kama Puff Daddy, yuko jela mimi niko njee, kuna L Kelly majina makubwa wao wako ndani.”
Chid Benzi, kwenye mahojiano na Millard Ayo alifunguka. Zaidi, anasema ni moja ya wasanii walioanza kushika pesa wakiwa na umri mdogo huku akiendelea kukazia kuwa hakumbuki ni vipi aliingia kwenye madawa.
Chanzo: Millard Ayo