Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Fid Q, Ay Watua Grammy

Wasanii nguli wa HipHop nchini Fareed Kibanda anayefahamika kama Fid Q na Ambwene Yesaya anayefahamika kama Ay wameandika historia mpya juu ya muziki wa wao na muziki wa Bongo Fleva kwa ujumla baada ya baada ya kuingia kwenye mchujo wa Tuzo za Grammy mwaka huu.

Kupitia mitandao yao instagram wasanii hao Oktoba 2,2025, waliuweka umma wazi juu nyimbo zao kupitishwa na Taasisi ya Recording katika kipengere cha Best African Music Perfomance.

Anaandika Fid Q “This isn’t just my win, it’s ours. From Tz to UG to the world, we’re making history together.” akiwa na maana ya kwamba Si ushindi wake pekee bali wa wote kutoka Tanzania mpaka Uganda kwenda Duniani, tutantengeneza historia yetu pamoja.

Ujumbe wa Fid Q, ukiwa unasadifu kuwa wimbo wake wa Glory 2, aliomshirikisha Damian Soul pamoja na msanii nguli toka Uganda Jose Chameleone ndio umefanikisha kupenye kwenye kipengere cha Best African Music Perfomance.

Kwa upande wa msanii Ay alichapisha kwa  kusema “Officially! Grammy has approved two of my entries for consideration for nomination. This is huge, not just for me na Harmonize but for Bongo Fleva and the entire Industry.” Akiwa na tafsiri ya Grammy imethibitisha nyimbo zake mbili si hatua kwake pekee yake na Harmonize bali kwa Bongo Fleva na kiwanda cha muziki kwa ujumla.

Ay akaendelea kwa kusema “Hizi project hazina global producer wala artists but pure Bongo and neighboring Country Tanzania na Zambia.”

Si wasanii wa kwanza toka Tanzania kukumuisha kuwa sehemu ya mchatao msanii Diamond Platnumz, mwaka 2020 alifanikisha kuingiza nyimbo mbili “Jeje na Baba Lao” 

Zaidi ikumbukwe, Tuzo hizo zitakuwa za 68 na zinatarajiwa kufanyika Februali, 2026 katika Jiji la Los Angles, Marekan huku Tanzania ikiwa haijawahi kupokea tuzo yeyote toka Grammy zianzishwe mwaka 1959.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: