Msanii maarufu Tanzania wa miondoko ya HipHop Ayubu Ibrahim Mndingo, Country Wizzy, anasema anajua watu wengi watamsifia siku ambayo hatakuwepo duniani kutokana na kipaji chake, uwezo wake na aliyoyafanya kimuziki.
Kwenye post yake mpya Instagram Country Wizzy ameandika "Najua mtanisifia sana nikifa, basi kabla sija-dead wakubwa statement official video iko Youtube".
"Halafu niwaambie tu nina mzuka mwaka huu, Promota piga simu na ukipiga simu hakikisha wasanii wako wote waimbe, mi mwaka huu wote nataka niimbe Dakika 40/ 1 hour Hapo yani".
Pia Country Wizzy ameongeza kueleza kuwa ata-performe Live Band kila show ili kuweka heshima na thamani ipande hataki kuimba Dk 10 wala 30 ni saa 1 stejini.
Chanzo; Eatv