Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wasanii Tz Waangukia Pua Tuzo za Grammy

Rasmi sasa Orodha ya wasanii kutoka Afrika iliyofanikiwa kuingia kwenye kipengele cha Best African Perfomer kimetoka na wasanii kutoka Tanzania hakuna hata mmoja.

Waliongia ni: - Love - Burna boy (Nigeria)
With you - Davido (Nigeria)
push to start - Tyla (Afrika Kusini)
Hope & Love - Eddy Kenzo (Uganda)
Gimme Dat - Ayrastarr ft Wizkidayo (Nigeria)

Kwa Tanzania Wasanii Saba (7) walifanikiwa kuingia kwenye Considerationya (kuzingatiwa) Grammy na orodha imetoka hakuna hata mmoja kutoka Tanzania ila Eddy Kenzo wa Uganda yupo kwenye kipengele.

Msanii Diamond alizingatiwa na GRAMMY kupitia wimbo wa Low aliowhirikishwa na Ciara kutoka Marekani na uliwekwa kwenye Kipengele cha Best African Performer na haujaingia, kwa Harmonize alizingatiwa katika nyimbo nne ambazo ni “Me Too ft Abigail Chams, Simuoni aliyoshirikishwa na AY, Furaha, na Finally aliyomshirikisha Miri Ben-Ari zote hazijaingia.

Fidq alizingatiwa kupitia wimbo wa Glory2 aliowashirikisha Damian Soul na Jose Chamilione kutoka Uganda na haujaingia.

Marioo alizingatiwa kupitia wimbo wa Nairobi na haupo pia Abby Chams alizingatiwa kupitia wimbo wa Me Too nao haupo.

Kwa upande wa Ay alizingatiwa kupitia nyimbo 2 ambazo ni Simuoni aliomshirikisha Harmonize na Wanga Neka aliomshirikisha Kanjiba kutoka Zambia na zote hazipo.

Kwa Afrika Mashariki Eddy Kenzo pekee kutoka Uganda ndio amefanikiwa kuingia kwenye kipengele aliwa na wasanii wa Nigeria kama Burna boy, Ayra Starr ft Wizkid, Davido ft Omah lay na Tyla kutoka Afrika Kusini

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: