Rapa Wa Marekani Lil Uz Vert Ameripotiwa Kushtakiwa Na aliyekuwa msaidizi wake binafsi “Symere Bysil Woods”, ambaye anadai kwamba alipata msongo wa mawazo na mateso ya kiakili alipokuwa akifanya kazi na msanii huyo kwenye ziara yake.
Mwanamke huyo anadai pia alipewa kauli chafu na vitendo vya kingono visivyotakiwa kutoka kwa Uzi.
Katika malalamiko yake, anasema alipewa nafasi ya kuwa msaidizi wa Uzi mwaka 2022 baada ya msanii huyo kuvutiwa na huduma zake alipokuwa akifanya kazi katika duka la Balenciaga huko Los Angeles.
Baada ya kuanza kazi, anadai alikumbana na mazingira ya kazi yaliyokuwa magumu, yenye shinikizo kubwa, na hata ya uhasama, huku Uzi akimnyanyasa kwa kauli na matendo yasiyofaa. Anaongeza kuwa baadhi ya wanachama wa timu ya usimamizi wa Uzi (Roc Nation) walihusika au walifumbia macho tabia hiyo.
Hivyo anadai alipitia unyanyasaji wa kimwili, kihisia na wa kingono wakati akifanya kazi kwa Uzi, na sasa anatafuta haki kupitia mahakama.
Chanzo; Wasafi