Staa wa vichekesho Bongo, Lucas Mhavile 'Joti,' amesema anapokuwa lokesheni kwa ajili ya kazi zake anaweza kuzingua na yeyote kama hawafahamiani endapo ataleta utani.
Joti ambaye aliwa hi kutesa na kikundi cha vichekesho cha Ze Komedi na Orijino Komedi, aliliambia Mwananchichi huwa anakua mtu mwingine kabisa na hata moyo wake unakuwa mgumu kwa sababu kwenye kazi huwa hatani, ni kazi-kazi.
Alisema wasanii wanapokuwa lokesheni, mambo mengi hutokea ikiweo kutania lakini kwake ingawa ni mchekesha ji na mpenda utani lakini si lokesheni.
"Unajua ninapokuwa lokesheni ndiyo nakua natengeneza mkate wangu, sasa mtu anaponiletea utani kwenye mkate wangu hapo hatuwezi kuelewana na uk weli lokesheni huwa sihitaji masihara kabisa," alisema Joti ambaye amejizolea umarufu pia kutokana na kazi zake za mitandaoi hasa YouTube na kubeba tuzo kadhaa zinazomdhihirisha ni mmoja wa wachekesha ji wakubwa zaidi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.
Chanzo: Mwananchi Scoop