Hivi karibu muigizaji kutoka nchini Marekani, Angelina Jolie ameviteka vichwa vya habari juu ya kinachoendelea kuhusu uhuru wa kujieleza huko nchini kwao. Mwigizaji aliulizwa kwenye tamasha la uzinduzi wa filamu yake ya “Couture” huko Hispania mwishoni mwa wiki, iliyopita “Kama msanii na Mmarekani, unaogopa nini?”
Jolie alijibu “Ni swali gumu,” kwamujibu wa gazeti la The Guardian akaendelea kusema “Ninaipenda nchi yangu, lakini kwa sasa, naona siitambui nchi yangu,”
“Sikuzote nimeishi maisha ya kimataifa; familia yangu ni ya kimataifa, marafiki zangu na maisha yangu ni ya kimataifa.”
Aliendelea kusema, “Mtazamo wangu unazingatia usawa, umoja, na mwelekeo wa kimataifa. Chochote popote duniani kinachogawanya watu au kuzuia uhuru wa kujieleza na uhuru wa mtu binafsi, nadhani ni hatari sana.”
Jolie akaendela , “Tunapoishi katika nyakati hizi za maana, lazima tuwe waangalifu tusiseme mambo kwa haraka au bila kufikiri. Hizi ni nyakati nzito sana ambazo tunazipitia pamoja.”
Maoni yake yanakuja baada ya kipindi cha usiku cha Jimmy Kimmel kuzimwa hewani na stesheni ya ABC bila kutaja muda wa kurudisha matangazo hayo, kutokana na mabishano yaliyosababishwa na maoni yake kuhusu kifo cha Charlie Kirk.
Chanzo: Tanzania Journal