Wizzy Mp Ajibu Vitisho vya Mashabiki wa Yanga Kumu-unfollow
Moja ya ua la rap linalozidi kumea vyema kila iitwapo leo, Tanzania, huwezi kuacha kulitaja jina la Wizzy Mp, rapa aliyejizolea umaarufu kwa namna yake ya kuwafikishia mashabiki zake burudani mpaka sehemu walipo.
Rapa huyo mwenye utaratibu wake wa kutembea na spika maarufu “BeatBox” mtaani huku akichana, amefunguka kilichotokea baina yake na mashabiki wa klabu ya Yanga kumtishia kumu-unfollow mara baada ya kutumbuiza kwenye tamasha la Simba Day 2025.
“Nafanya muziki ili maisha yangu yaende nikisema sifanyi show ya Simba kwasababu mashabiki wa Yanga watani-unfollow itakuwa haina maana ya mimi kufanya muziki, ipo siku watanielewa kwanini nimefanya.”
Zaidi , amefungukuwa comment za mashabiki wa Yangu kuhusu kumu-unfollow zilikuwa zinamtia unyonge, amefunga yote kwenye kipindi cha Bongo Fleva ya Clouds Fm, Septemba 27,2025.
Ikumbukwe, Wizzy Mp, ni moja ya wasanii wachanga waliotumbuiza kwenye matamasha makubwa ya vilabu nchini 2025, akiunga na Dogo Pateni, Mdogo Sajent na wengi neo.
Chanzo: Tanzania Journal
Video: Clouds Media