Msanii wa Bongo Fleva, Jux amekutana na mtoto wake Rakeem kwa mara ya kwanza.
Jux amechapisha baadhi ya video akimpokea mkewe Priscy na mtoto wao Rakeem ambaye alizaliwa Agosti 24, 2025, nchini Canada.
Tangu Priscilla ajifungue huko nchini Canada, Jux hakubahatika kumuona mtoto wake ana kwa ana. Sambamba na hayo Jux aliandaa surprise kibao kwa mkewe na mtoto baada ya kuwasili nyumbani.
Zaidi, mpaka sasa wawili hao hawajaiweka wazi sura ya mtoto wao tangu azaliwe.
Chanzo: Mwananchi Scoop