Nicki Minaj ameendelea kuwashutumu watu mbalimbali kupitia mitandao yake ya kijamii ikiwemo mtandao wa X, hivi karibuni amezungumzia sababu ya ugomvi wake na Jay-Z.
Ambapo, Jumatano, Oktoba 1, Nicki alidai kuwa Jay-Z alikasirika kwa sababu alikataa kumpa mdundo “beat” ambayo tayari alikuwa ameanza kufata taratibu za kisheria kwa ajili ya wimbo wake"Thought I Knew You," uliotoka mwaka 2018 akimshirikisha The Weeknd.
Katika tweet yake kwenye mtandao wa X, Nicki aliandika: "Jay-Z alikasirika kwa sababu sikumpa beat ambayo tayari nilikuwa nimeanza taratibu za kisheria. Wimbo huo nilioufanya na The Weeknd kwenye albamu yangu ya Queen, Alisema ni beat ya Beyonce na Hoeberson, alikubali tu kuwapa na kisha kunishtaki kwa kufanya beat inayofanana."
Nicki pia anaamini kuwa Jay-Z ana wivu na Nas. Alisema: "Jay-Z ana wivu sana na Nas. Nilishtakiwa kwa mamia ya maelfu ya dola kwa wimbo nilioufanya na Nas, ambao haujawahi kutoka rasmi, Casino."
Akaendelea kuwa wakati yeye na Nas walipokuwa wakipiga picha za video kwa kutumia magari ya zamani, Jay-Z alionekana akipiga picha akiwa mtaani ‘hood’ akiwa na magari ya zamani pia.
Historia kati ya Jay-Z na Nas sio mpya, kwani wawili hao wamewahi kuwa na migogoro ya muda mrefu ambayo baadaye ilisuluhishwa.
Chanzo: Tanzania Journal