Usiku wa kuamkia leo, Desemba 30, 2025, mwanamuziki Harmonize alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake mwigizaji Kajala Masanja. Hata hivyo, tukio hilo limezua gumzo kubwa mitandaoni baada ya wawili hao kutoruhusu picha wala video za tukio la kuvishana pete kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu ambacho kilihudhuria katika tukio hilo kilieleza kuwa Paula ambaye ni mtoto wa Kajala alipokonya simu za watu wote ambao walialikwa katika tukio hilo ili wasipige picha wala video na kuwa tukio hilo litapostiwa na wahusika wenyewe muda ukifika.
Sherehe hiyo ambayo ilifanyika katikati ya Bahari kwenye Yatch ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Paula mtoto wa Kajala, Lamata, Mwijaku, Gara B na wengineo wengi.
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo, Harmonize ameeleza vitu ambavyo amekuwa akivikumbuka kutoka kwa Kajala baada ya kuachana naye ni kuwa ni ukaribu wake pamoja na sapoti aliyokuwa akimuonesha.
“Nilimisi vitu vingi lakini cha umuhimu zaidi ni utu wake, utu wake unanifanya nakuwa 'serious', utu wake unanifanya nakuwa 'hard work', unanipa utulivu, utu wake unanipa utulivu wa kufikiria maisha, kingine ameifanya my house kuwa home, akiwa nyumbani kwangu yaani kunageuka kuwa nyumbani nikisema hivi nadhani kila mtu ananielewa,” amesema Harmonize.
Aidha wakati tukio hilo likiendelea wawili hao walifichua kuwa watafunga ndoa mwaka 2026 huku hashtag yao rasmi ikiwa ni #HK4ever.
Chanzo; Mwananchi Scoop