Mwanamuziki Nasib Abdul, Maarufu Diamond Platnumz, ameendelea kuthibitisha ubora wake kimataifa baada ya kutangazwa rasmi kuwa sehemu ya albamu ya wimbo wa mashindano ya AFCON 2025, yanayoendelea kufanyika Morocco.
Albamu hiyo yenye nyimbo 12 imewakutanisha wasanii wakubwa wa kimataifa na barani Afrika akiwemo Ne-Yo, Davido, French Montana, Ayra Starr, Rema, Jason Derulo, Shenseea, Saad Lamjarred, Akon, Yemi Alade, Patoranking, Innos’B, na wengine wengi.
Chanzo; Clouds Media