Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Safari Mpya ya Kajala na Harmonize Ilikotokea

Mwigizaji mkongwe nchini Kajala Masanja amefichua kuwa hajaanza uhusiano na mwanamuziki Harmonize hivi karibuni na badala yake walianza muda mrefu tangu Paula yupo Sekondari.

Akizungumza kwenye kipindi chao cha ‘A LIST’ ambacho kinaruka YouTube Kajala ameeleza kuwa ameanza uhusiano na Konde muda mrefu huku akisisitiza kuwa Harmo aliwahi kumlipia ada Paula.

“Yaani watu wasichokijua nilianzaga na Harmonize muda mrefu sana. Mimi Harmo ashamlipia Paula ada sijui ya Form Two, nilikuwa sina ada alinipa ada na kipindi hicho ndio kwanza ameanza muziki, alikuwa bado mdogo kabisa.

“Nikamwambia mwezio nina shida Paula amerudishwa nyumbani hana ada nakumbuka mtoto wa watu alienda benki Kijitonyama akanipa hela barabarani pale Bamaga. Kwa hiyo nilifanya mambo mengi sana kuhakikisha Paula anasoma,”amesema Kajala

Utakumbuka uhusiano wa wawili hao ulitambulika katika mitandao ya kijamii mapema mwaka 2021 na baada ya hapo waliachana. Lakini huo haukuwa mwisho wao walirudiana tena mwaka 2022 ambapo walirudi kwa kishindo na Harmonize kumvisha pete Kajala.

Tukio ambalo lilifanyika Juni 25, 2022 katika hoteli ya Serena na kulipa jina la ‘Late Lunch’ huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwamo uongozi wa lebo ya Konde Gang, Mkurugenzi wa TVE, Francis Ciza ‘Majizzo’, Aunty Ezekiel, Martin Kadinda na wengineo.

Wawili hao walichumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu walipotengana baada ya mwanamuziki huyo kumfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu.

Aidha, licha ya kurudiana kwao penzi hilo lilivunjika tena miaka miwili iliyopita na kila mmoja akafuata njia yake. Lakini sasa wameibua tena mjadala kutokana na mabusu waliyopigana katika show ya Konde iliyofanyika Zanzibar Desema 25. Hata hivyo safari yao ilianza tena kwa kuvishana pete tukio ambalo lilifanyika Usiku wa kuamkia, Desemba 30, 2025.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: