Muigizaji Wa ‘Black Panter' Marehemu Chadwick Boseman kutunukiwa nyota kwenye Hollywood Walk of Fame, Novemba 20 mwaka huu. Taarifa hii imethibitisha na mandao wa Variety leo. Chadwick Boseman Alifariki Dunia Agosti 2020 Akiwa Na Umri Wa Miaka 43 Kufuatia Maradhi Ya Saratani yaliyokuwa yakimkabili. Chadwick alifahamika zaidi kutokana na uchezaji wake kama ‘King T’chala’ katika filamu ya Black Panther Lakini Pia baada ya kujiunga na kampuni ya Marvel Cinematic Universe mwaka 2016 na kushiriki katika filamu za Captain America; Civil War, Avengers Infinity War na nyingine nyingi.
Chanzo; Wasafi