Wakati mwanamuziki Sean “Diddy” Combs, akiendelea kutumikia kifungo chake gerezani. Hali sio shwari kwa familia yake ambapo inaelezwa mali na fedha zote za rapa huyo zipo chini ya uangalizi mkali, wa kampuni ya usimamizi wa biashara ya Tri Star Sports & Entertainmen. Hivyo watoto hawawezi kutumia fedha bila kutoa taarifa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka TMZ inaeleza watoto wa Diddy hawawezi kutumia fedha za baba yao kama ambavyo walikuwa wakitumia hapo awali na badala yake kila jambo lina bajeti yake maalumu na matumizi yoyote yaliyo nje ya bajeti yanawasilishwa katika kampuni hiyo.
Aidha inasemekana hadi mambo madogo kama chakula kwa ajili ya familia yanahitaji kuwasilishwa kwa kampuni na mara nyingine maombi hayo yalikataliwa, jambo ambalo limekuwa likiifanya familia hiyo kuishi maisha magumu ambayo hawajayazoea.
Zaidi ya hayo, baadhi ya wafanyakazi wa Diddy na mawakili wake wamesema hawajalipwa kwa wakati. Jambo ambalo limepelekea kuacha kazi, licha ya kutuma taarifa zao za malipo katika kampuni ya ‘Tri Star Sports & Entertainmen’.
Sean “Diddy” Combs ana watoto saba ambao ni Quincy Taylor Brown (alizaliwa 1991), Justin Dior Combs (1993), Christian “King” Combs (1998), Chance Combs (2006), mapacha D’Lila Star Combs na Jessie, James Combs (2006), pamoja na Love Sean Combs (2022). Watoto aliowapata kwa wanawake tofauti.
Ikumbukwe Sean “Diddy” Combs alikamatwa na mamlaka za Marekani Septemba 16,2024 katika moja ya hoteli iliyopo Manhattan, New York. Baada ya mchakato wa kisheria, kesi ilianza kwa uchaguzi wa majaji Mei 5, 2025, na Julai 2, 2025 alikutwa na hatia kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa shughuli za ngono.
Chanzo; Mwananchi Scoop