Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wasanii Watengewa Mabilioni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ametangaza uwepo wa kiasi cha Sh20 bilioni ambazo zitagawanywa kwa makundi tofauti kwenye sekta za michezo, sanaa na utamaduni ili kuhakikisha zinapiga hatua.

Makonda ameyasema hayo jana Februari 16, 2026 katika hafla fupi ya Kocha Miguel Gamondi kusaini mkataba wa kuinoa Taifa Stars, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

"Katika bilioni 20 (shilingi), tumepewa mgawanyo. Ndio maana ndani yake tukapata zile Sh2 bilioni kwa ajili ya watengeneza maudhui.

"Lakini pia ziko kwenye upande wa muziki, ziko kwenye upande wa filamu. Kwa hiyo Katibu Mkuu ataainisha makundi yote ambayo yatakwenda kupokea fedha kutoka kwetu," amesema Makonda.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: