Msanii Naseeb Abdul, maarufu Diamond Platnumz amejitokeza hadharani kukanusha tetesi zinazovumishwa ndani ya mitandao ya kijamii kuwa ameongeza mke wa pili.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anafahamika kama mume halali wa msanii Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu, amechapisha andiko la kanusho masaa kadhaa mara baada ya kuachia video ya
wimbo wake mpya unaotambulika kama “Msumari”
“Naona kuns misumari inapigiliwa kuwa Simba kaongeza mke, hapana sijaongeza msinipe ujasiri nisio kuwa nao.” - Diamond
Akaendelea kwa kujibu dhidi ya video inayotanda ikimuonyesha yupo na mwanamke kwenye gari “Clip nyingine inasambaa niko na kwa gari na msichana, hiyo ni video yangu nyingine, mambo ya ugomvi na wife sitaki.” - Diamond
Ikumbukwe, Diamond Platnumz ni moja kati ya wasanii wachache Afrika na Tanzania wenye uwezo wa kuteka mashabiki wake kwanzia mtindo wake wa maisha, mahusiano, nyimbo zake na hata mitindo yake ya nguo.
Chanzo: Tanzania Journal