Mwigizaji maarufu wa Hollywood, Sylvester Stallone ambaye anafahamika kwa jina la Rambo ameripotiwa kuikosoa hafla ya Tuzo za Grammy za mwaka huu, akidai kuwa zimepoteza mvuto na lengo kuu la kusherehekea muziki.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini humo Stallone ametoa ya moyoni akieleza kuwa tuzo za mwaka 2026 ziliboa kwani zilitawaliwa na ajenda za kisiasa badala ya Sanaa na ubunifu wa wasanii.
Mbali na hilo amemkosoa pia mshereheshaji wa tuzo hizo Trevor Noah, akimtaja kuwa ametia aibu, huku baadhi ya mashabiki mitandaoni wamemnanga Noah wakieleza kuwa utani na kauli alizozitoa hazikufaa kabisa kutolewa katika hafla hiyo.
Inaelezwa kuwa baada ya hafla hiyo kurushwa hewani, mitandao ya kijamii imejaa malalamiko kutoka kwa watazamaji wakidai Grammy zimepoteza mvuto wake wa awali kwani waandaji wamekuwa wakizingatia vitu visivyo na msingi huku wakiacha kuenzi muziki na wasanii wake.
Licha ya lawama hizo, waandaaji wa Grammy pamoja na Trevor Noah bado hawajatoa tamko rasmi kujibu shutuma zinazozidi kuongezeka. Ikumbukwe hafla ya ugawaji tuzo za Grammy ilifanyika Februari 1, 2026, katika jijini la Los Angeles.
Chanzo; Mwananchi Scoop