Streamer maarufu Duniani IshowSpeed ameaga rasmi baada ya kumaliza ziara yake Barani Afrika, akitoa shukrani zake kwa mataifa 24 aliyoyatembelea pamoja na Tanzania licha ya kuwa hakuweza kufika nchini Tanzania ujumbe ambao umegusa moyo mioyo ya watu mbalimbali baada ya kufanya matangazo ya moja kwa moja (streams) katika nchi 20 nzuri za Afrika ndani ya siku 28 tu
Kitendo cha IshowSpeed kuitaja Tanzania kwenye shukrani zake imeonesha kuwa Speed ameona support kubwa ya Watanzania katika Live stream zake hasa alipotembelea Kenya ambapo aliandika rekodi kubwa zaidi ya mapokezi ya ziara yake jambo ambalo limeonesha ishara njema huwa dunia ikamshuhudia akitembelea Tanzania kwenye ziara zake za awamu ijayo.
Ziara hii ilimwezesha Speed kuonyesha sura halisi na nzuri ya bara la Afrika ambayo mara nyingi vyombo vya habari huificha mbele ya dunia sambamba na kuonesha maendeleo ambayo Afrika inayo kwasasa sambamba na kuelimisha dunia juu ya historia, tamaduni, mila na maisha ya Waafrika kwa ujumla.
Chanzo; Crown Media