Mwanamuziki maarufu wa Nigeria, Damini Ebjnoluwa Ogulu almaarufu Burna Boy, amethibitisha kuwa 'amesilimu' na kuhamia katika dini ya Kiislamu na kuitwa jina la Abdulkarim na kueleza kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kupata “amani na utulivu wa kiroho” alipokuwa akijifunza kuhusu imani hiyo.
Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni, Burna Boy alisema alikulia katika familia ya Kikristo, lakini utafiti na tafakari binafsi zimemfanya ajikute akivutiwa na mafundisho ya Uislamu.
“Nilizaliwa Mkristo, lakini sasa nimekubali Uislamu. Nilihisi amani ya ndani na kuelewa zaidi maana ya maisha,” alisema msanii huyo katika mahojiano yaliyosambaa mitandaoni.
Chanzo; Global Publishers