Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

P Diddy Atuma Barua kwa Jaji Kabla ya Hukumu Dhidi Cassie

Kuelekea kwenye hukumu yake P Diddy, awasilisha barua kwa Jaji wa kesi yake  Arun Subramanian, akiomba msamaha dhidi ya tukio lake na Cassie ambapo kwenye barua hiyo mfanyabiahara na msanii P Diddy ameonyesha wazi jinsi gani anajutia kitendo kile.

 "Picha na tukio la kumpiga Cassie zinarudia kichwani mwangu kila siku. Niliipoteza akili yangu kabisa. Nilifanya makosa makubwa kuweka mikono juu ya mwanamke niliyempenda.”

“Samahani kwa hilo na nitasikitika daima. Vurugu zangu za nyumbani zitabaki kuwa mzigo mzito ambao nitawahi kubeba milele." Alimaliza P Diddy. 

Kuelekea kwenye hukumu ya Oktoba, 3,2025 Ijumaa, mapema timu ya P Diddy iliachia video ya dakika 11 inayoonyesha vipande vya video ya P Diddy akiwa na  watoto wake pamoja na video za zamani zake akifanya mambo mazuri na watu wakimsifu. Video za sasa za watoto wake wakimtumia meneno ya faraja na kumtia moyo.

Hukumu ya P. Diddy au Sean Combs, inahusu makosa mawili ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono (transportation to engage in prostitution), kinyume na Sheria ya Mann Act ya huko Marekani na hukumu yake inatarajiwa kusomwa tarehe 3 Oktoba 2025 mjini New York, ikiwa ni miezi mitatu baada ya kukupatikana na hatia ya makosa mawili.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: