Mwigizaji na Mwongozaji wa filamu za Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’ amefichua siri ya ndoa yake kudumu kwa miaka 17 sasa, huku akitaja mapenzi kwa mkewe na mambo mengi yameifanya izidi kustawi na hajui kitu kurogwa.
Akizungumza na Mwananchi, Cheni ambaye anatamba na filamu na tamthilia nyingi Bongo, amesema watu wengi ndoa zao zinayumba kwa sababu ya namna wanavyoishi, tofauti na yeye ambaye amekuwa msaada mkubwa kwake na hasa kazi za nyumbani.
Amesema katika ndoa yake, anajiona mshindi kwani mbali na mapenzi anayopata kwa mkewe, pia ni pambo na anahitaji kusaidiwa, naye anatekeleza mambo yote muhimu kwake.
“Mwanamke ni kama pambo, hili wanaume wengi hawalitambui,” amesema na kuongeza; “Kuna baadhi ya kazi ambazo wanawake wanafanya, lakini hawakupaswa kabisa kuzifanya.”
Amefichua kazi hizo baadhi ni kupika na kufua, akibainisha kwamba anachotakiwa mwanamke ni kupata raha na kumshauri mwanaume wake katika mambo mengine huku akisema mwanamume anapaswa kuzifanya kazi za ndani akiwa na mke ama mpenzi wake.
Chanzo; Mwananchi Scoop