Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mahakama Yamfutia Kesi Nyota wa Squid Game

Nyota wa Squid Game, O Yeong-Su ameachiwa huru na mahakama kutoka nchini Korea Kusini baada ya kuhukumiwa kifungo kufuatia na kesi ya unyanyasaji wa kijinsia tukio ambalo lilitokea mwaka 2017.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 81 alishtakiwa mwaka 2022 kwa kumkumbatia mwanamke ambaye jina lake halikuwekwa wazi na kumbusu kwenye shavu bila ridhaa yake.

Mwaka 2024 alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi minane lakini siku ya Jumanne Novemba 11,2025 mahakama ilibatilisha kifungo chake ikieleza kuwa tayari mwigizaji huyo amepata mufunzo kuhusu unyanyasaji wa kingono.

Mahakama imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 2017 wakati Su alipokuwa kijijini kwenye maonyesho ya ‘Tiyatro’, mwanamke huyo alifungua kesi hiyo 2021 lakini awali kesi hiyo ilifungwa Aprili mwaka huo huo na baadaye upande wa mashtaka ulifungua upya uchunguzi kwa ombi la mlalamikaji.

Mahakama ya Wilaya ya Suwon imeeleza kuwa ilikuwa inamashaka kama kweli Su amefanya unyanyasaji huo huwenda kulikuwa na taarifa za upotoshwaji hivyo imechukua uamuzi wa kumuachi huru.

Kwa upande wa mwanamke huyo ameikosoa hukumu hiyo akisema haitafuta ukweli au kufuta maumivu aliyoyapata. “Licha ya hukumu ya leo, nitaendelea kusema ukweli hadi mwisho,” alisema kupitia shirika la haki za wanawake Womenlink.

Ikumbukwe, Bwana O alipata umaarufu baada ya kuigiza katika filamu ya Squid Game, na kupitia filamu hiyo mwaka 2022 ilimfanya kuwa muigizaji wa kwanza wa Korea Kusini kushinda Golden Globe ya mwigizaji bora wa pili katika mfululizo huo.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: