Katika moja ya mahojiano aliyofanya staa wa muziki Nigeria, Rema aliweka wazi vigezo anavyotaka kwa mwanamke.
Rema alieleza kuwa ikitokea anataka mwanamke wa kutoka nae kimapenzi, atazingatia ambaye haongei sana, haposti mitandaoni na mwenye wafuasi wachache.
Rema alisema akitaka kutafuta mwanamke, lazima awe na sifa hizo kwasababu hapendi mwanamke muongeaji. Kutweet sana na kuchapisha mitandaoni.
"Sipendi wasichana wanaotweet, kuongea, kupost sana. nikitaka kudate na mwanamke nitatafuta mwenye wafuasi wachache kama 1,000 au 500. Ambaye ukurasa wake wa Instagram upo private," amesema Rema.
Chanzo; Mwananchi Scoop