Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Latto Aanika Njee Mahusiano Yake na 21 Savage

Baada ya miaka ya uvumi na ushirikiano kadhaa wa kimuziki, rapa maarufu Latto amethibitisha kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na rapa 21 Savage.

Habari hiyo ilitolewa na Latto katika mahojiano na TMZ jijini New York, Jumatatu, Septemba 29.

Latto, mwenye umri wa miaka 26, alizungumza na TMZ kuhusu mitindo yake ya mavazi kabla ya kuthibitisha uhusiano huo, akisema yeye ni kama mke wa Mafia anayetamba kwenye mitaa ya New York.

“Sasa naenda kula chakula cha jioni na mume wangu,” alisema Latto.

Alipohojiwa kama amechoshwa na uvumi wa uhusiano wake na 21 Savage (jina lake halisi Shéyaa Bin Abraham-Joseph), Latto alijibu:

“Hapana. Ni mume wangu, mume wangu, mume wangu.”

marapa hawa walianza kuhusishwa kutoka kimapenzi tangu Desemba 2020, miezi michache baada ya kushirikiana kwenye wimbo wa Pull Up kutoka kwenye albamu ya Latto, Queen of da Souf.

Walirudia kushirikiana tena mwaka 2022 kwenye ngoma ya Wheelie kutoka kwenye albamu yake ya 777.

Mashabiki pia waligundua mwaka 2023 kuwa Latto alichora tattoo nyuma ya sikio lake iliyoonekana kuwa na jina la kwanza la 21 Savage, Shéyaa.

Hata hivyo, Latto aliendelea kuwa mgumu kuelezea maisha yake ya kimapenzi, akisema kwenye mahojiano ya Agosti 2024 na Apple Music:

“Mtandao haujui chochote. Sikiliza muziki na utajua unachohitaji kujua.”

 

Chanzo: Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: