Katika ulimwengu wa burudani, mapenzi ya wasanii yamekuwa yakivutia hisia za mashabiki wao, huku baadhi huonekana kuishi katika uhusiano wenye misukosuko ya kuachana na kurudiana mara kwa mara.
Tabia hiyo mara nyingi inachangiwa na wivu, umaarufu na mambo mengine.
Hivi karibuni, uhusiano wa masupastaa Wema Sepetu na Oscar John Lelo maarufu Whozu au Chibaba umekuwa gumzo miongoni kwa mashabiki na mitandao ya kijamii, baada ya kukumbwa na misukosuko hiyo.
Uhusiano wa Wema na Whozu umekuwa ukizungumzwa sana kuhusu kuachana na kurudiana na wiki chache zilizopita kila mmoja aliweka wazi kuwa wameachana, lakini watu walikuwa wakisubiri jibu la kurudiana.
Sasa sikia hii! Wema amelitonya Mwananchi juzi kuwa wamerudiana na Chibaba wake.
“Ni kweli sikuwa sawa na mwenzangu Whozu. Mimi huwa nikikwazika, na mtu anayenifahamu anaweza kunielewa kuwa huwa naweza kuzungumza kitu chochote bila kujali baadaye itakuwaje. Hasira zangu zikiisha, huyo mtu ninayekwazana naye nakuwa mwepesi wa kusameheana. Hivyo sijaona tatizo kusameheana na Whozu ikiwa tayari tumeshakuwa wapenzi wa muda mrefu; kifupi tuna historia kwa watu,” alisema Wema na kuongeza:
Chanzo; Mwananchi Scoop