Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki (CCM), Hamis Taletale, akichangia mjadala wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13, ameomba kuwepo na mabadiliko ya sheria yatakayowawezesha wasanii kukopa fedha kupitia Mfuko wa Sanaa bila riba na masharti magumu ya dhamana, tofauti na ilivyo sasa ambapo mikopo hiyo hutolewa kwa kufuata taratibu za kibenki.
Taletale amesema mfumo uliopo kwa sasa hauwapi fursa wasanii wengi kunufaika na fedha zinazotolewa na Serikali kama ilivyokuwa awali wakati ikitolewa kutokana na vigezo vinavyowataka kuwa na mali kama nyumba ili kupata mkopo.
“Kama kuna utaratibu wa kisheria sisi ndio watunga sheria. Nakushauri Waziri Makonda leteni sheria hapa ili tuwasaidie wasanii. Kama kuna utaratibu wa kukopesha hizi pesa ambazo Mhe. Rais amezileta wapewe. Kama utaratibu huu ni mgumu ambao mmeujengea, ukitaka kukopa pesa ambayo ameileta Rais eti mnataka niweke nyumba, si kila msanii ana nyumba” Hamis Taletale (Babu Tale) - Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki.
Chanzo; Millard Ayo