Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Stromae wa “Papaoutai” Wimbo wa “Baba Uko Wapi”

Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii kama Instagram na TikTok basi utakuwa umekutana na wimbo uitwao ‘Papaoutai’, ambao umekuwa ukifanya vizuri huku mashabiki wakiutumia katika mambo mbalimbali bila kujua maana halisi ya wimbo huo.

Papaoutai wimbo ambao umeimbwa na stromae, uliachiwa mwaka 2013, mpaka kufikia sasa umetazamwa zaidi ya mara Bilioni 1.1 katika mtandao wa YouTube. Huku ukikadiliwa kupata ongezeko la wafuatiliaji kutokana na wimbo huo kuwavutia watu mbalimbali duniani kote.

Papaoutai ni wimbo unaoeleza maisha halisi ya msanii huyo ukiwa na maana ‘Baba Uko Wapi’. Uliachiwa mahususi kwa ajili ya kumuenzi baba yake ambaye alifariki dunia katika Mauaji ya Kimbari. Wimbo huo aliuimba akielezea panda shuka ambazo alikumbana nazo katika malezi yake pamoja na ndugu zake tangu baba yake afariki dunia.

Aidha baada ya kuachia wimbo huo vyombo vya habari mbalimbali vilifanya mahojiano naye kutaka kujua kwa undani historia yake ambapo amekuwa akieleza kuwa dhumuni la kuachia wimbo huo ni kutaka kujua jukuma la baba kwa familia yake.

“Nilikuwa najaribu tu kuuliza, jukumu la baba ni nini hasa? Kwa upande wa maisha yangu binafsi, ni kweli sikumfahamu sana baba yangu. Swali kubwa ni baba mzuri ni yupi, baba ni nani, na baba mbaya ni yupi? Na ukweli ni kwamba, sote tunajaribu tu kufanya tuwezavyo.

 

 

Chanzo; Mwananchi Coop

Kuhusiana na mada hii: