Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Urusi Kuimarisha Ushirikiano Baina ya Vijana na Tanzania

Urusi imeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya vijana wa nchi hiyo na Tanzania ili kuendeleza undugu uliodumu kwa muda mrefu.

 

Hayo yamesemwa na Vakhtang Khiklandze ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kurugenzi ya World Youth Festival wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum ya kuhitimishwa kwa kongamano la World Youth Festival Assembly lililofanyika katika jiji la Niznhy Novrogod, Urusi.

Akijibu swali aliloulizwa na Shafii Mpanja kutoka Clouds Media alietaka kujua vijana wengi zaidi ambao hawakubahatika kufika kwenye kongamano hilo watapataje fursa ya kujifunza, Khiklandze amesema tayari kurugenzi hiyo imeandaa mpango wa kufungua klabu za World Youth Festival Assembly kwa kila nchi ambapo kupitia klabu hizo zitatengenezwa programu za kufikia vijana wengi zaidi wa Kitanzania.

“Tumejizatiti katika kuimarisha ushirikiano baina ya vijana wa Urusi na Tanzania na tayari tunawasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ili kulifanikisha, lakini kuna kitu kimoja ambacho kiko wazi ni kwamba tunapozungumza kwa haya makongamano tunaongea moja kwa moja na waliopo na tunapokubaliana kuwa miradi ya kuanzisha tunawasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ili kuisimamia”.

Khiklandze amesema pia katika kuenzi ushirikiano baina ya Tanzania na Urusi, tayari kuna makala fupi inayoandaliwa yenye historia wa mataifa hayo mawili ambayo itaonyeshwa kupitia kwa ubalozi wa Urusi Tanzania kwa kushirikiano na Russian Cultural Centre.

Kongamano la World Youth Forum Festival lilioandaliwa na Shirikisho la Masuala ya Vijana (Rosmolodezh), kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Niznhy Novgorod limehitimishwa rasmi Jumamosi Septemba 20 baada ya kufanyika kwa siku 5 mfululizok likiwakutanisha vijana 2000 toka mataifa mbalimbali likilenga kufungua ushirikiano baina ya vijana duniani kote ambapo mada mbalimbali kuhusu ujasiriamali, ubunifu, vyombo vya habari na masuala ya kijamii.

Kuhusiana na mada hii: