Baada ya ukimya wa muda mrefu kufuatia kilichotokea katika ghasia siku za Uchaguzi Mkuu, kuchomewa duka lake la Nenga Tronix, msanii BillNass ame-share video ya sehemu ya hasara ambayo amepata.
Kupitia Whatsapp Status, BillNass ame-share clip inayoonyesha baadhi ya Simu, Laptop, na pesa ambazo zilifanikiwa kuokolewa baada ya kuchomwa moto kwa duka hilo, kwa maneno machache akionyesha ishara ya shukrani kwa Mungu wake kufuatia jaribu hilo kwa kuweka emoji za 🙏🏾🙏🏾
BillNass alifunga ukurasa wake wa Instagram mara tu baada ya kupatwa na changamoto hiyo!
Chanzo; Clouds Media