Ishowspeed akiwa kwenye ziara yake Afrika ameweka rekodi ya kuwa Youtuber wa kwanza ku-steam katika Pyramids za Misri.
YouTuber maarufu wa Marekani IShowSpeed (Darren Jason Watkins Jr.) ameingia katika historia ya utiririshaji wa moja kwa moja (live stream) akiwa ndani ya Piramidi ya Giza, Misri kitu ambacho hakijawahi kufanywa na stremer mwingine yeyote kabla yake.
Hii ni sehemu ya “Speed Does Africa” tour yake ya siku 28 kote Afrika, ambapo anafanya livestream ya safari yake na watu wengi wakiangalia mtandaoni.
Chanzo; Bongo 5