Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Rose Muhando Aibuka na Madai Mazito ya Kudhulumiwa

Msanii maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania, Rose Muhando, ameibuka hadharani na kutoa malalamiko mazito kuhusu kile alichokitaja kuwa ni kudhulumiwa haki yake ya mapato kutokana na kazi zake za muziki katika majukwaa ya kidijitali.

Kupitia taarifa yake, Rose Muhando amesema kwa takribani miaka 15 amekuwa akinyamaza na kuvumilia kwa moyo wote, akiamini kuwa haki yake ingetendeka, lakini maumivu aliyoyapitia yamemlazimu sasa kufungua mdomo na kusema.

Msanii huyo amesema changamoto hiyo inatokana na ushirikiano wake wa zamani na kampuni moja, akieleza kuwa licha ya kuachana na kampuni hiyo kitambo, hadi sasa bado inashikilia zaidi ya kazi zake 37 na kukataa kuziachia.

Ameongeza kuwa cha kusikitisha zaidi ni kwamba hapati hata shilingi moja kutokana na kazi hizo, ilhali ni jasho lake na jasho la maisha yake.

Rose Muhando amebainisha kuwa Serikali kupitia COSOTA, imekuwa ikijaribu kumsaidia na kusimamia haki yake, lakini juhudi hizo zimekwama kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa mwakilishi wa kampuni hiyo ambaye amekuwa akiitwa mara kadhaa bila kutoa ushirikiano wowote.

Ameeleza kuwa hali hiyo imemuumiza sana, imemvunja moyo na kurejesha nyuma ndoto za wasanii wengi ambao, kwa mujibu wake, wanaendelea kudhulumiwa haki zao kimyakimya katika tasnia ya muziki.

Kwa unyenyekevu, Rose Muhando ameomba Serikali iingilie kati suala hilo kwa haraka, akimtaja moja kwa moja Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ili kuhakikisha haki inatendeka.

 

 

Chanz; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: