Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Dolph Lundgren na Miaka Miwili ya Kuishi Baada ya Saratani

Mwigizaji maarufu wa filamu za mapigano kutoka Sweden, Dolph Lundgren, amewahi kupitia kipindi kigumu cha maisha baada ya kugundulika kuwa na saratani ya figo, ugonjwa ambao madaktari waliwahi kumwambia amebakisha miaka miwili ya kuishi.

Nyota huyo anayefahamika zaidi kupitia filamu za mapigano za Hollywood, alifichua kuwa ugonjwa huo ulianza mwaka 2015 alipogundulika na uvimbe kwenye figo wakati alipokwenda hospitali kwa lengo la kucheki afya yake.

Kwa mujibu wa maelezo yake, madaktari walibaini uvimbe huo mapema na akafanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu iliyokuwa imeathirika. Baada ya matibabu hayo, hali yake ilionekana kuimarika na aliendelea na kazi zake za uigizaji bila kuweka wazi hadharani kuhusu changamoto aliyokuwa akipitia.

Hata hivyo, mwaka 2020 hali ilibadilika ghafla baada ya vipimo vipya kuonesha kuwa saratani ilikuwa imerudi na kuenea katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo ini, tumbo pamoja na maeneo ya karibu na mapafu.

Lundgren alisema taarifa hiyo ilikuwa pigo kubwa kwake na familia yake, hasa baada ya madaktari kumpa makadirio ya kuishi ikiwa ni miaka miwili hadi mitatu, jambo ambalo lilimfanya aanze kufikiria mustakabali wa watoto wake na maisha yake binafsi.

“Niliwaza namna ya kuwaeleza watoto wangu kuhusu hali halisi. Ilikuwa ngumu kuamini,” aliwahi kueleza katika mahojiano yake.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: