Kutoka Nigeria msanii Davido amechaguliwa kuwa sehemu ya wadau wa Grammy Awards watakao wapigia kura wasanii ili waweze kushiriki kwenye vipengele mbalimbali vinavyowafaa.
Davido kwenye moja video clip mara baada ya kuthibitishwa kuwa sehemu ya mchakato amesema” Kuelewa umuhimu wa sauti zetu zinavyosikilizwa na kushiriki katika mchakato wa Tuzo za Grammy ni mabadiliko makubwa.”
Pamoja na kuamini ni mabadiliko makubwa katika muziki Afrika aliongezea kwa kusema “Nimejifunza jinsi kupiga kura kunavyokuwezesha kuwa na sauti katika kile kinachozingatiwa na kupigiwa kura kila msimu wa tuzo.” - Davido
Chanzo: Tanzania journal