Muimbaji Wa Nigeria ‘Kizz Daniel’ amevunja ukimya na kujibu madai ya kuchelewa kwenye show yake huko paris, Nchini Ufaransa Jana Hadi Kupelekea Vurugu kati ya mashabiki na waandaji wa show yake.
Kupitia IG Story Yake Kizz Daniel Amesema; “Kwanza Kabisa Hili Halikuwa Kosa Langu, Kwani Video Zote Mnazoziona Ni bifu Kati Ya Wakala Wa Ziara Yangu Olamide Baron Pamoja Na Promoter Wa Show”.
“Nililipwa kuja kutumbuiza Paris Na Olamide Baron Kikamilifu, Akauza Show Kwa Promoter Mwingine, Na Kwa Mujibu Wake Promoter Huyo Alivunja Mkataba Kwa Kutomlipa Pesa Zake…(Nitapost Na Mkataba huo uliovunjwa).”
“Binafsi Nilikuwa Tayari Tangu Saa 12:00 Asubuhi Kwa Ajili Ya Ndege Ya 6:25 Mchana…. Nilikuwa na Kaka yangu Adesope Hotelini, Kwani Tulicheleweshwa Ndege Na Olamide Baron Ili Aweze Kulipwa Pesa Zake Kwanza. Jambo ambalo sikuwa na fahamu kabisa. Hata hivyo alimaliza masuala yake na promoter lakini hatukuweza kuiwahi ndege. Na ndege iliyofuata ilitoka Saa 11:25 Jioni … Hivyo tulichelewa paris Kwasababu Ya Matatizo ya promoters Wawili” - Kiss Daniel
Chanzo; Wasafi