Muimbaji wa R&B kutoka Marekani, R. Kelly anaripotiwa kuwekwa chini ya uchunguzi katika gereza la shirikisho lililopo North Carolina baada ya kupatikana na namba ya simu ya mkuu mstaafu wa gereza hilo.
Kwa mujibu wa wakili wake, Kelly amewekwa katika hali ya kutengwa (isolation) kwa muda wote wa uchunguzi huo ukiendelea.
Hatua hiyo imechukuliwa kama sehemu ya taratibu za kiusalama za gereza na mamlaka zikichunguza namna namba hiyo ilivyopatikana na iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za mawasiliano kwa wafungwa.
Mpaka sasa mamlaka za gereza hazijatoa taarifa rasmi kuhusu matokeo ya awali ya uchunguzi huo.
Wakili wa msanii huyo ameeleza kuwa mteja wake anashirikiana na uchunguzi unaoendelea.
R. Kelly kwa sasa anatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kesi za makosa ya kingono na usafirishaji haramu wa watu.
Chanzo; Bongo 5